Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:33

Samsung kusitisha uzalishaji Galaxy Note 7


Simu ya Samsung ya Galaxy Note 7.
Simu ya Samsung ya Galaxy Note 7.

Samsung kusitisha utengenezaji wa simu ya Galaxy Note 7 kutokana na sababu za kiusalama.

Kampuni ya inayotengeneza vifaa vya kielektroniki ya Samsung ilioko Korea kusini imesema inapunguza utengenezaji wa simu iliotatizika ya Galaxy Note 7 ili kuhakikisha usalama wake.

Mapema Jumatatu, shirika la habari ya Korea kusini lilimnukuu muuzaji moja wa simu hizo akisema kuwa Samsung ilikuwa imesitisha utengenezaji wa simu aina ya Note 7 kufuatia masharti yaliotolewa mashirika yanayolinda usalama wa watumizi wa bidhaa kutoka Korea Kusini, Marekani na China kufuatia ripoti kuwa maduka ya simu Marekani yamesitisha uuzaji wa simu hizo kutokana na sababu za kiusalama.

Kasoro kwenye simu hiyo aina ya Note 7 imeacha kampuni hiyo ikiwa kwenye tatizo kubwa zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka mingi. Simu aina ya Samsung Note 7 zimekuwa sikishika moto tangu zilipozinduliwa mwezi Agosti.

XS
SM
MD
LG