Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 11:25

Rwanda yashutumu DRC kwa kurusha kombora katika ardhi yake


wanajeshi wa DRC wakiwa katika mapumziko baada ya kupambana na waasi wa FDLR. Feb, 27 2015
wanajeshi wa DRC wakiwa katika mapumziko baada ya kupambana na waasi wa FDLR. Feb, 27 2015

Jeshi la Rwanda limeshutumu jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa kurusha kombora ndani ya Rwanda, lililojeruhi raia kadhaa.

Msemaji wa jeshi la Rwanda Col. Ronald Rwivanga, amesema kwamba maafisa wa jeshi wanashirikiana na maafisa wa jeshi la DRC kuchunguza kisa hicho kilichotokea katika wilaya ya Musanze.

Rwanda inataka uchunguzi wa kina kufanyika.

Baadhi ya maafisa wa DRC wameshutumu jeshi la Rwanda kwa kuunga mkono makundi ya wapiganaji yanayotekeleza mashambulizi mashariki mwa Congo, ambapo kuna utajiri mkubwa wa madini.

Rwanda imetaja madai ya kuunga mkono makundi ya waasi nchini Congo kuwa yasiyokuwa ya msingi.

Mapigano makali yanaendelea kati ya wanajeshi wa DRC na wapiganaji wa kundi la M23.

XS
SM
MD
LG