Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 10, 2025 Local time: 21:21

Rwanda yasema raia kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na wanajeshi wa DRC


Map of Rwanda
Map of Rwanda

Rwanda Jumatatu ilisema raia kadhaa walijeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya kuvuka mpaka yaliyoendeshwa na wanajeshi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuomba “uchunguzi wa haraka” kuhusu tukio hilo.

Mizinga ya roketi ilianguka katika wilaya ya kaskazini ya Musanze, inayopakana na DRC, “na kujeruhi raia kadhaa na kuharibu mali”, jeshi la Rwanda limesema katika taarifa.

Urushaji wa makombora hayo ulitokea Jumatatu asubuhi na kudumu dakika 21, jeshi limesema bila kutoa maelezo zaidi.

“Hali katika eneo hilo ni ya kawaida na usalama umeimarishwa,” msemaji wa jeshi la Rwanda Kanali Ronald Rwivanga alisema.

Rwanda imesema iliomba tume ya mseto ya kikanda ya waangalizi wa kijeshi wanaofuatilia matukio ya kiusalama kwenye mpaka, kuendesha uchunguzi wa haraka.

“Maafisa wa Rwanda wanawashirikisha pia wenzao wa DRC kuhusu tukio hilo,” Rwivanga alisema.

Jeshi la DRC lilikuwa bado kutoa maelezo kuhusu madai hayo.

XS
SM
MD
LG