Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:14

Rwanda yaanza utoaji chanjo dhidi ya Marburg


Mhudumu wa afya akijiandaa kwa utoaji wa chanjo.
Mhudumu wa afya akijiandaa kwa utoaji wa chanjo.

Rwanda ilisema Jumapili imeanza kutoa dozi za chanjo dhidi ya virusi vya Marburg ili kujaribu kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa kama wa Ebola katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ambapo hadi sasa umeua watu 12.

"Chanjo inaanza leo," Waziri wa Afya Sabin Nsanzimana alisema katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Kigali.

Alisema chanjo hizo zitazingatia wale "walio hatarini zaidi, wafanyikazi wa afya walio katika hatari zaidi wanaofanya kazi katika vituo vya matibabu, hospitalini, ICU, katika dharura, lakini pia wanafamilia wa karibu wa watu waliothibitishwa kuambukizwa.

Nchi hiyo tayari imepokea shehena ya chanjo hizo zikiwemo kutoka Taasisi ya Sabin Vaccine.

Mlipuko wa kwanza wa homa hiyo ya virusi ya kuvuja damu nchini Rwanda uligunduliwa mwishoni mwa mwezi Septemba, na visa 46 na vifo 12 vimeripotiwa tangu wakati huo. Marburg ina kiwango cha vifo hadi 8asili mia 88, kwa mujibu wa watyaalam wa afya.

Dalili za Marburg ni pamoja na homa kali, maumivu makali ya kichwa na udhoofikaji wa jumla wa afya ndani ya siku saba baada ya kuambukizwa na baadaye kichefuchefu kikali, kutapika na kuhara.

Forum

XS
SM
MD
LG