Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 13:43

Ruto ametupilia mbali mswada wa fedha - kubana matumizi, kusitisha miradi ya maendeleo


Rais wa Kenya Dr. William Ruto akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Nairobi - June 26, 2024
Rais wa Kenya Dr. William Ruto akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Nairobi - June 26, 2024

Rais wa Kenya Dr. Willam Ruto ametupilia mbali mswada wa fedha wa 2024 uliozusha utata na maandamano makubwa nchini humo na kusababisha vifo na uharibifu wa mali.

Akihutubia taifa kutoka Ikulu ya Nairobi, Ruto amesema anakubali kwamba wananchi wametoa kauli yao na amewasikia.

Ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya serikali, Ruto ametangaza hatua mbali za kupunguza matumizi ya pesa ikiwemo kusitisha miradi mbalimbali ya maendeleo, kupunguza bajeti katika ofisi ya Rais, wizara mbalimbali, bajeti ya bunge na serikali za kaunti.

Aidha ameeleza kwamba kwa kila shilingi mia moja ya kenya inayokusanywa, shilingi sitini na moja zinatumika kulipa madeni na kwa hivo itabidi wakenya kuishi kulingana na uwezo wao katika nchi hiyo yenya mzigo mkubwa wa madeni, ambapo asilimia 60 ya bajeti inatumika kulipa madeni.

Rais Ruto ameashiria kusitisha mipango ya kuajiri walimu, kuunganisha umeme, bima ya afya kwa kila raia huku akisisitiza kwamba atalinda viwanda vya ndani dhidi ya uangizaji wa biadha ambazo Kenya ina uwezo wa kutegeneza.

Forum

XS
SM
MD
LG