Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:52

Russia yaushambulia kwa makombora mji wa Ukraine wa Lviv na kusababisha ukosefu wa umeme


Magari yaliyoharibiwa na makombora ya Russia katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Oktoba 10, 2022. Picha ya AP
Magari yaliyoharibiwa na makombora ya Russia katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Oktoba 10, 2022. Picha ya AP

Shambulio la kombora la Russia kwenye miundo mbinu muhimu mjini Lviv leo Jumanne limesababisha ukosefu wa umeme katika sehemu ya mji huo wa magharibi mwa Ukraine, meya wa mji huo Andriy Sadovyi amesema.

Shahidi aliyezungumza na shirika la habari la Reuters ameripoti milipuko miitatu mjini humo muda mfupi baada ya saa sita mchana majira ya huko.

Sadovyi ameandika kwenye ujumbe wa telegram kwamba “ kutokana na shambulio hilo la kombora, asilimia 30 ya mji wa Lviv hauna umeme kwa muda,” akiongeza kuwa usambazaji wa maji umesitishwa katika wilaya mbili za mji.

Mtandao wa usambazaji wa umeme katika mkoa wa Lviv ulishambuliwa pia na makombora ya Russia siku ya Jumatatu.

Viongozi wa mji huo walisema baadaye Jumatatu kwamba umeme umerejea katika sehemu kubwa ya mkoa huo, lakini naibu waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine, Yevheniv Yenin, amesema baadhi ya maeneo ya mkoa huo yalikuwa hayana umeme Jumanne asubuhi.

XS
SM
MD
LG