Finland ambayo inashirikiana mpaka na Russia wenye urefu wa kilomita 1,300, pamoja na Sweden zinatafakari kujiunga na muungano wa NATO.
Finland itachukuwa uamuzi wiki zijazo, waziri mkuu Sanna Marin alisema Jumatano.
Dmitry Medvedev ambaye ni naibu mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Russia, amesema iwapo Sweden na Finland zitajiunga na NATO basi Russia italazimika kuimarisha vikosi vyake vya nchi kavu, majini na angani katika bahari ya Baltic.
Medvedev pia ameelezea wazi tishio la nyuklia kwa kusema kwamba hakutokuwa tena na mazungumzo ya Baltic “isiyo na nyuklia” ambapo Russia ina eneo lake la Kaliningrad kati ya Poland na Lithuania.
“Hatuwezi tena kuwa na mazungumzo juu ya hadhi ya kutokuwa na nyuklia kwa Baltic, usawa lazima urejeshwe,” amesema Medvedev, ambaye alikuwa rais wa Russia kuanzia 2008 hadi 2012.