Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 29, 2024 Local time: 12:55

Russia yataka kulipiza kisasi kwa Marekani


Russia imeahidi hatua za kulipiza kisasi kwa Marekani Jumatatu, kwa kumwita balozi wa Marekani, Lynne Tracy, kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na kuilaumu Marekani kwa kuishambulia Crimea inayokaliwa na Russia.

Russia inadai kuwa shambulizi hilo lilimetekelezwa kwa makombora yaliyotolewa na Marekani.

“Hatua za kulipiza kisasi hakika zitafuata,” Wizara ya Mambo ya nje ya Russia, imesema licha ya kutotoa taarifa zaidi. Russia imesema mifumo ya makombora kutoka jeshi la Marekani, inayofahamika kama ATACMS, ulitumika katika shambuliz hilo lililouwa takriban watu wanne na kujeruhi 150.

John Bass, naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anayehusika na masuala ya kisiasa, ameiambia VOA kuwa hafahamu idadi ya vifo vya shambulizi hilo, lakini amesema kumekuwa na tofauti kubwa katika jinsi Ukraine na Russia, zinavyofanya mashambulizi yao.

Forum

XS
SM
MD
LG