Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 21:42

Russia yashambulia mji aliozaliwa rais wa Ukraine


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema shambulizi la anga la Russia, lilipiga mji aliozaliwa wa Kryvyi Rih kusini mwa Ukraine, Jumatano, na kuua takriban watu wanane na wengine 21 kujeruhiwa.

Rais Zelenskyy alionyesha video iliyochukuliwa na idara ya huduma za dharura ikimuonyesha mtu akiwa amebebwa kwenye machela na maafisa wa zima moto huku moshi ukifuka kutoka kwenye majengo yaliyoharibiwa.

Miongoni mwa yalioharibiwa ni pamoja na jengo la ofisi la ghorofa. Wakati huo huo, maafisa katika eneo la Belgorod, Russia, wamesema makombora ya Ukraine yameua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu.

Vyacheslav Gladkov, gavana wa mkoa huo, amesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba shambulizi hilo lilifanyika katika mji wa Shebekino, ambao uko karibu na mpaka wa Ukraine.

Mashambulizi hayo pia yaliharibu majengo ya makazi, Gladkov amesema.

Forum

XS
SM
MD
LG