Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 01:58

Russia yaituhumu Ukraine kuushambulia mji wa Moscow kwa kutumia ndege isiyo na rubani


Picha hii iliyochukuliwa kwa video inaonyesha kifaa kinacholipuka angani na kutoa mwanga mkubwa juu ya jengo la baraza la Seneti la Kremlin wakati wa shambulio la drone linalodaiwa kufanywa na Ukraine, Mei 3, 2023.
Picha hii iliyochukuliwa kwa video inaonyesha kifaa kinacholipuka angani na kutoa mwanga mkubwa juu ya jengo la baraza la Seneti la Kremlin wakati wa shambulio la drone linalodaiwa kufanywa na Ukraine, Mei 3, 2023.

Russia imesema Ukraine ilifanya shambulizi la ndege isiyo na rubani Jumanne dhidi ya Moscow, huku wanajeshi wa Russia wakiendesha shambulizi la anga la 17 mwezi huu dhidi ya mji mkuu wa Ukraine.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema kuwa aidha ilizitungua au kuzizuia ndege nane zisizo na rubani ambazo zilikuwa zinailenga eneo la Moscow.

Meya wa Moscow Sergei Sobyanin amesema shambulizi hilo liliharibu majengo mawili ya makazi na kujeruhi watu wawili.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba Rais Vladimir Putin alipewa taarifa kuhusu hali hiyo.

Maafisa wa Ukraine walikuwa hawajatoa maelezo kuhusu madai hayo ya Russia.

Shambulio hilo linafuatia lile la mapema mwezi Mei ambalo maafisa wa Russia walisema liliilenga Kremlin. Russia iliituhumu Ukraine kwa shambulio hilo.

Mapema Jumanne, Russia ilifanya kile maafisa wa Ukraine walichokiita shambulio kubwa lililoulenga mji wa Kyiv kwa kutumia zaidi ya ndege 20 zisizo na rubani ambazo ziliharibiwa na mifumo ya ulinzi ya Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG