Wizara ya mambo ya nje ya Marekani haikutoa mara moja maelezo juu ya madai ya kuwanyima visa wanahabari hao.
“Marekani inachukulia kwa uzito mkubwa wajibu wake kama nchi mwenyeji wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa mkataba wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo kutoa visa,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje alisema katika taarifa.
Wanahabari hao walikuwa na lengo la kufuatilia kuwepo kwa Lavrov kwenye jukwaa la Umoja wa mataifa kuashiria uenyekiti wa Russia kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Akizungumza kabla ya kuondoka Moscow jana Jumapili, Lavrov alisema “ Nchi inayojiita yenye nguvu zaidi, yenye akili zaidi, huru na ya haki imejitokeza na kufanya jambo la kijinga kwa kuonyesha kile ambacho iliapa kuhusu kulinda uhuru wa kujieleza na kupata habari ni mambo muhimu.”
Amesema “muwe na uhakika kwamba hatutasahau na hatusamehe.”