Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 02:12

Russia yafungia baadhi ya vyombo vya habari vya Ulaya


Russia, Jumanne imesema ilikuwa inapiga marufuku kuingia nchini humo kwa matangazo ya vyombo 81 tofauti vya habari kutoka Umoja wa Ulaya vikiwemo AFP na Politico ikiwa ni kulipiza kisasi marufuku kama hiyo ya Umoja wa Ulaya kwa vyombo kadhaa vya habari vya Russia.

Umoja wa Ulaya mwezi Mei ulitangaza kusitisha usambazaji wa kile ulichokitaja kuwa mitandao minne ya propaganda inayohusishwa na Kremlin, na kuondoa haki zao za utangazaji ndani ya umoja huo.

Ulisema wakati huo marufuku hiyo ililenga Sauti ya Ulaya, shirika la habari la RIA, na magazeti ya Izvestia na Rossiyskaya Gazeta.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Jumanne imejibu kwa kutoa orodha ya vyombo 81 vya habari kutoka nchi 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya, pamoja na vile vya Ulaya, ambavyo matangazo yake imesema hayatapatikana tena katika eneo la Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG