Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:25

Russia, Ukraine wanajitayarisha kwa mapambano makali Kherson kila upande unatoa madai ya ‘bomu chafu’


Wanajeshi wa Ukraine kwenye magari ya kijeshi, Novoselivka, Sept. 17, 2022
Wanajeshi wa Ukraine kwenye magari ya kijeshi, Novoselivka, Sept. 17, 2022

Wanajeshi wa Russia wanajitayarisha kwa mapigano makali zaidi katika mji wa Kherson, kusini mwa Ukraine wakati utawala wa Kremlin ukilenga kuulinda kwa nguvu zote mji huo mkubwa ulio chini ya udhibithi wake.

Wanajeshi wa Russia katika eneo hilo wamekuwa wakilazimika kurudi nyuma kutokana na mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine katika siku za hivi karibuni.

Wanakabiliwa na hatari ya kukwama katika ukingo wa mto Dnipro kwa upande wa magharibi, ambapo mji mkuu wa Kherson umekuwa mikononi mwa Russia tangu walipoivamia Ukraine miezi 8 iliyopita.

Maafisa walioteuliwa na Russia kusimamia eneo hilo wamekuwa wakiwahimiza wakaazi kuhamia ukingo wa mashariki, lakini Oleksiy Arestovych, mshauri wa rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, amesema kwamba hakuna ishara za wanajeshi wa Russia kutaka kuachilia mji huo.

"Kuhusu mji wa Kherson, kila kitu kipo wazi. Wanajeshi wa Russia wanajipanga upya na kujiimarisha,” amesema Arestovych akiongezea kwamba “ina maana kwamba hakuna anayetaka kujiondoa. Mapigano makali kabisa yatatokea Kherson.”

Kati ya mikoa minne ambayo rais wa Russia Vladimir Putin alitangaza kujitengea kimabavu kutoka kwa Ukraine mnamo mwezi Spetemba, Kherson unatajwa kuwa ndio muhimu zaidi kimkakati.

Kherson ndio njia pekee ya kufikia Crimea kwa barabara. Crimea ni eneo ambalo Russia ilinyakua kimabavu kutoka kwa Ukraine mwaka 2014.

Mwanachama wa baraza la utawala la Ukraine katika eneo la Kherson, ambalo liliondolewa madarakani kufuatia mapinduzi ya Russia, Yuri Sobolevsky, amesema kwamba maafisa wa Russia wamekuwa wakiwalazimisha wakaazi wa Kherson kuhamia nchini Russia.

Russia imesema kwamba inawahimisha watu kwa ajili ya usalama wao.

Mahangaiko ya wakaazi wa Kherson

Viktor Palyanitsa akiwasha moto kwa ajili ya kupata joto nyumbani kwake Kurylivka, Ukraine, Oct. 16, 2022
Viktor Palyanitsa akiwasha moto kwa ajili ya kupata joto nyumbani kwake Kurylivka, Ukraine, Oct. 16, 2022

Mwandishi wa shirika la habari la Reuters ambaye yupo safu ya mbele ya mapigano kati ya wanajeshi wa Russia na Ukraine, ameripoti kwamba hakuna makombora au ushambuliaji wa risasi uliripotiwa Jumanne, na wakaazi wa sehemu hiyo wamesema kwamba wanaomba sana mapigano yakome na wanajeshi wa Russia kuondoka Kherson.

"Unalala usiku bila kujua kama utaamka ukiwa hai,” amesema Mikola Nizinets, mwenye umri wa miaka 39.

Mfumo wa umeme na gesi umeharibiwa katika sehemu hiyo na wakaazi hawana chakula cha kutosha.

Katika sehemu za kaskazini mashariki, wanajeshi wa Russia wanaendelea kudhibithi miji ya Bakhmut ulio kwenye barabara kuu kueleea miji ya Sloviansk na Kramatorsk, eneo la Donetsk region.

Madai ya ‘bomu chafu’

Russia imeambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba Ukraine inapanga kutumia “bomu chafu”, madai ambao yamefutiliwa mbali na mataifa ya magharibi Pamoja na maafisa wa Ukraine kwamba ni uongo unaotumiwa na Russia ili kuendelea kupigana.

Naibu wa balozi wa Russia katika umoja wa mataifa Dmitry Polyanskiy, amesema kwamba Ushahidi wao umetolewa kwa mataifa ya magharibi.

"Sijali watu wakisema kwamba Russia inalalamika iwapo hilo halitatokea kwa sababu hili ni tukio baya zaidi, lenye uharibifu mkubwa na linalotishia dunia nzima,” ameambia waandishi wa habari.

Rais Zelenskiy amesema kwamba madai ya Russia yanaashiria kwamba Moscow inapanga kutumia silaha ya kimkakati na baadaye kulaumu Ukraine.

Russia imekanusha madai hayo.

Rais wa Marekani Joe Biden, amesema kwamba Russia itakuwa imefanya makosa makubwa sana, iwapo itatumia silaha ya kimkakati.

Wachunguzi wa nyuklia wa UN

Baraza la usalama la umoja wa mataifa katika kikao Sept 7,2022
Baraza la usalama la umoja wa mataifa katika kikao Sept 7,2022

Katika hatua ya kujibu madai ya Russia, baraza la nyuklia la umoja wa mataifa limesema kwamba linapanga kutuma wataalam katika sehemu mbili za Ukraine ambazo hazijatajwa, kufanya uchunguzi.

Wataalam watatumwa kufuatia ombi la serikali ya Ukraine.

Tangu wanajeshi walipopata pigo kubwa mwezi Septemba, Putin ameamurisha kuongezwa wanajeshi wa Russia nchini Ukraine.

Maelfu ya wanajeshi wa akiba wametumwa Ukraine, kutangaza kujitengea kimabavu sehemu 4 za Ukraine, na hoja ya matumizi ya silaha za nyukilia kuanza kusikika kila mara.

XS
SM
MD
LG