Mazungumzo hayo ambayo yamechapishwa na serikali ya Russia, yanaeleza kwamba Shoigu amemwambia mwenzake wa Ufaransa kwamba wana wasiwasi mkubwa huenda Ukraine ikatumia “bomu chafu” katika vita hivyo.
Russia haijatoa ushahidi wowote kuonyesha kwamba Ukraine inaweza kutumia silaha kama hiyo.
"Wamezungumzia hali ilivyo nchini Ukraine ambayo inaendelea kuharibika kwa haraka,” imesema taarifa ya wizara ya ulinzi ya Russia na kuongezea kwamba “inaelekea kuwa mbaya kiasi cha kudhibitiwa.”
Wizara ya ulinzi haijatoa taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo.