Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 05:39

Russia na Ukraine zote zadai kushikilia mji karibu na Donetsk


Russia na Ukraine zimetoa madai yanayo kinzana Jumapili, ni taifa lipi linadhibiti eneo  karibu na mji wa, Blahodatne, ulioko masharimi mwa mkoa wa Donetsk.

Kundi la mamluki wa kijeshi la Russia, Wagner, limedai kushikilia udhibiti wa kijiji, huku jeshi la Ukraine likisema vikosi vyake vilizima shambulizi.

Mkuu wa utawala wa vikosi vya jeshi la Ukraine, amesema katika ripoti ya kila siku kwamba jeshi la Ukraine, lilizima mashambulizi ya vikosi vya uvamizi katika maeneo ya Blahodtne.

Pia Ukraine imesema pia ilizima mashambulizi ya Russia katibu na makazi 13 katika mkoa wa Donetsk.

Lakini kundi la Wagner, ambalo limetangazwa na Marekani kama la uhalifu wa kimataifa, limesema kupitia ujumbe wa Telegram ambapo ni App ya kutumiana ujumbe kwamba kikosi chake kimechukua udhibiti wa Blahodatne, Jumapili.

XS
SM
MD
LG