Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:40

Russia na Ukraine zimerushiana makombora kuelekea kila upande


Wanajeshi wa Ukraine wakirusha makombora
Wanajeshi wa Ukraine wakirusha makombora

Jeshi la Ukraine limesema kwamba limetungua ndege zisizokuwa na rubani 18 kati ya 19 zilizorushwa na Russia katika mashambulizi ya leo usiku yaliyolenga sehemu za katikati na magharibi mwa Ukraine.

Mfumo wa ulinzi wa Ukraine umeangusha ndege hizo katika mikoa ya Dnipropetrovsk, Mykolaiv, Odesa, Ternopil na Vinnytsia.

Russia vile vile imerusha makombora ya masafa marefu kuelekea Peninsula ya Crimea.

Gavana wa Odesa Oleh Kiper, ameandika ujumbe wa Istagram kwamba shambulizi hilo limedumu kwa saa kadhaa.

Ameripoti kwamba shambulizi la ndege zisizokuwa na rubani limesababisha moto kwenye ghorofa tatu katika jengo la makazi, mjini Chornomorsk, sawa na jengo lenye ofisi za wilaya ya Odesa.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema kwamba imeangusha ndege zisizokuwa na rubani 14 za Ukraine katika mkoa wa Belgorod, uliopo kwenye mpaka wa Russia na Ukraine, pamoja na ndege nyingine mbili kwenye Black Sea.

Forum

XS
SM
MD
LG