Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 03:10

Russia kushambulia zaidi mashariki mwa Ukraine


Mkaburi ya kuwazika watu wanaofariki kutokana uvamizi wa Russia nchini Ukraine. April 14 2022 Picha: AP
Mkaburi ya kuwazika watu wanaofariki kutokana uvamizi wa Russia nchini Ukraine. April 14 2022 Picha: AP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenzky amesema kwamba wanajeshi wa Russia wanajitayarisha kushambulia sehemu za mashariki mwa nchi hiyo na kutoa wito kwa raia wa Ukraine kutotii amri za wanajeshi hao.

Zelensky ametoa wito kwa mataifa ya magharibi kupiga marufuku ununuzi wa mafuta ya Russia akisema kwamba hatua hiyo ni muhimu sana, wakti uvamizi wa Russia nchini Ukraine ukiingia siku ya 54.

Rais Volodymyr Zelensky ameshutumu Russia kwa kile ametaja kama kutaka kuharibu eneo zima la mashariki, la Donbas, lenye bandari muhimu ya Maripol.

Amesema hayo wakati jeshi la Ukraine likijitayarisha kulinda eneo hilo.

Moscow inapigana kudhibithi mji wa kusini wakati ikiimrisha mashambulizi kudhibithi Donbas na kufungua njia kuelekea sehemu ya Crimea ambayo tayari inadhibithi.

"Wanajeshi wa Russia wanajitayarisha kutekeleza mashambulizi mashariki mwa nchi katika siku chache zijazo. Wanataka kuharibu kabisa Donbas. Wanataka kuharibu kila kitu ambacho kilikuwa Fahari ya eneo hili la viwanda. Namna wanajeshi wa Russia wanavyoharibu Mariupol, ndivyo wanataka kuharibu miji mingine na jamii katika mweneo ya Donetsk na Luhansk. " amsesema Zelensky

Kiongozi huyo wa Ukraine ameapa kwamba nchi yake itapigana na kulinda Mariupol, akikaidi amri ya Russia ya kutaka wanajeshi wa Ukraiane walio katika kiwanda cha kutengeneza chuma cha Azovstal, kujisalimisha.

Mariupol imekumbwa na mapigano makali na kuzuia wanajeshi wa Russia kupiga hatua, tangu Russia ilipovamia Ukraine, Februari 24.

Maafisa wa Ukraine wametoa wito kwa watu wa Donbas kuhamia sehemu za magharibi ili kuepuka mashambulizi makali ya wanajeshi wa Russia , katika jaribio lao la kutaka kudhibithi sehemu za Donetsk na Lugansk.

Hii leo, wanajeshi wa Russia wamepiga sehemu kadhaa za Ukraie huku wakipanga wanajeshi wake kadhaa kutekeleza mashambulizi makubwa katika sehemu za mashariki.

Shambulizi kubwa limetokea magharibi, saa chache baada ya rais Zelensky kuishutumu Moscow kwa kupanga kuharibu kabisa sehemu yote ya mashariki.

Katika sehemu magharibi, gavana Maksym Kozytsky ameandika kwenye kurasa za kijamii kwamba makombora manne ya Russia yamesababisha uharibifu mkubwa mjini humo.

"Watu saba wamekufa, 11 kujeruhiwa na kwa sasa, mabaki ya nyumba yanaendelea kutolewa. Kuhusiana na shambulizi lililopiga karakana ya magari, shambulizi hilo ni utovu mkubwa uliolenga raia waliofika kazini kufanya kazi zao."

Mashambulizi ya kumatatu yamefanyika wakati Russia imeongeza mashambulizi katika sehemu za mashariki za mji mkuu wa Kyiv, yakilega viwanda vya kutengeneza silaha.

Mshambulizi hayo vile vile yanafanyika baada ya Moscow kuapa kupngeza mashambulizi zaidi katika mji mkuu, kujibu kile maafisa wa kijeshi wa Russia wamedai kwamba Ukraine ilitekeleza mashambulizi kwenye ardhi yake, Pamoja na kuzamisha meli yake ya vita - Moskva.

XS
SM
MD
LG