Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:33

Russia kufanya maonyesho ya kijeshi wakati inakabiliwa na wasiwasi kuhusu usalama wa ndani


Manowari ya Russia ikishiriki katika mazoezi ya kijeshi ya Russia Oct. 26, 2022
Manowari ya Russia ikishiriki katika mazoezi ya kijeshi ya Russia Oct. 26, 2022

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema leo Ijumaa kwamba tangazo la hivi karibuni la Russia kwamba manowari inayotumia nguvu za nyuklia haitatumika wakati wa maadhimisho ya siku ya jeshi la majini la nchi hiyo huenda inatokana na kufanyiwa ukarabati na wasi wasi uliopo.

Maadhimisho hayo yatakayofanyika St. Petersburg, Julai 30.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema hayo katika ripoti yake ya kila siku kuhusu vita vya Russia nchini Ukraine.

Hata hivyo, wizara hiyo vile vile imesema kwamba kuna uwezekano kwamba wasiwasi kuhusu usalama wa ndani ya Russia, tangu kundi la Wagner lilipojaribu kufanya mapinduzi, umechangia katika kuchukuliwa kwa uamuzi huo.

Ofisi ya rais wa Ukraine imesema Alhamisi kwamba mashambulizi ya Russia yameua raia watatu wa Ukraine na kujeruhi wengine 38

Serikali ya Ukraine imesema kwamba wanajeshi wa Russia wamelenga miji 13 na vijiji kadhaa vilivyo chini ya udhibithi wa Russia, katika mkoa wa mashariki wa Donetsk kwa kutumia makombora na mizingia mizito.

Watu 21 wamejeruhiwa Zaporizhzhia kutokana na mashambuzli ya ndege zisizokuwa na rubani, huku mfumo wa ulinzi wa Ukraine ukiangusha ndege hizo ambazo zililitengenezwa nchini Iran, na zilikuwa zimeilenga Kyiv.

Forum

XS
SM
MD
LG