Maafisa wa Ukraine wamesema kwamba utawala wa Moscow umeendelea kuangusha makombora nchini Ukraine na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa kwa siku ya nne mfululizo.
Russia imesema inaangusha makombora hayo nchini Ukraine kufuatia kuharibiwa kwa daraja linalounganisha Russia na Crimea.
Shambulizi karibu na mju mdogo wa Makariv, kilomita 50 magharibi mwa Kyiv, limeharibu miundo msingi.
Russia imeendelea kushambulia sehemu zinazokaliwa na raia huku wanajeshi wake wakiendelea kupoteza sehemu ambapo walikuwa wanashikilia nchini Ukraine.
Wafuasi wa rais wa Russia Vladimir Putin wamekuwa wakitaka rais huyo kuongeza kasi ya mashambulizi baada ya daraja la Crimea kushambuliwa.
Warusi wanapokea mafunzo kutoka kwa Iran
Maafisa wa Ukraine wamedai kwamba watu wa iran wnaaoishi katika sehemu za Ukraine zilizonyakuliwa na Russia kimabavu, walikuwa wanatoa mafunzo kwa wanajeshi wa Russia namna ya kutumia mifumo ya ulinzi ambayo inaweza kutekeleza mashambulizi ya angani na namna ya kulenga shabaha.
Ukraine imedai kwamba huenda jeshi la Russia limeishiwa na ndege zisizokuwa na rubani na sasa inapata msaada wa Iran.
Jeshi la Ukraine limesema kwamba mfumo wake wa ulinzi wa anga umeharibu ndege zita zisizo na rubani za Iran zilizokuwa zinapaa juu ya Odesa na Mykolaiv saa za usiku.
Spika wa bunge la chini la Russia amesema kwamba wanajeshi wa Russia wameshambulia zaidi ya mifumo 70 ya nshati ya Ukraine wiki hii.
Ametishia kwamba mashambulizi zaidi yataendelea kujibu mashambulizi ya Kyiv, japo Ukraine haijasema kama ilihusika na shambulizi la mabomu kwenye daraja.
Maafisa wa Russia wamesema kwamba wanajeshi wa Ukraine wameangusha makombora katika eneo la Belgorod, ndani ya Russia, karibu na Ukraine.
Gavana wa eneo hilo Vyacheslav Gladkov, amesema kwamba makombora hayo yameharibu nyumba inayokaliwa na watu katika mji wa Balgorod, huku kombora lingine likianguka katika uwanja wa michezo, japo halikulipuka.
Muungano wa NATO umesema kwamba unafuatilia mwenendo wa Russia, hasa baada ya Putin kusema kwamba atatumia kila njia kulinda Russia.