Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:51

Russia inatumia mamluki katika vita Ukraine, wanajeshi wa kawaida hawatoshi, hawana risasi


Mwanamme aliyefiwa na mtu wa familia yake kutokana na mashmabulizi ya makombora ya Russia katika mji wa Mykolaiv, Ukraine. Oct 13, 2022
Mwanamme aliyefiwa na mtu wa familia yake kutokana na mashmabulizi ya makombora ya Russia katika mji wa Mykolaiv, Ukraine. Oct 13, 2022

Ripoti ya ujasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema kwamba makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na Russia, yamepiga hatua kuelekea mji wa Bakhmut, eneo la Donetsk, katika muda wa siku tatu zilizopita.

Wizara hiyo imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba wapiganaji hao wamepiga pia hatua katika vijiji vya Opytine na Ivangrad, kuelekea kusini mwa mji huo.

Ripoti inasema wanajeshi rasmi wa Russia wamepiga hatua ndogo sana katika kudhibithi sehemu za Ukraine, tangu mwezi Julai.

Hata hivyo, ripoti hiyo inasema kwamba “wanajeshi wanaoongozwa na kundi la mamluki wa Russia la Wagner wamepiga hatua Donbas. Mamluki wa Wagner wanahusika sana katika mapigano ya Bakhmut.”

Ripoti inaendelea kusema kwamba “Russia inaamini kwamba kuudhibithi Bakhmut ni muhimu katika hatua yake ya kijeshi kuelekea Kramatorsk, inayoshikiliwa na Ukraine.”

Japo wanajeshi wa Russia wanaendelea kupigana katikati mwa Donbas, na wanapiga hatua za kujikokota sana, ujasusi wa Uingereza unasema kwamba “mashambulizi kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine yamedumaza mikakati yao hasa katika sehemu za kusini na kaskazini.”

Wanajeshi wa Russia pia wanakabiliwa na uhaba wa risasi na idadi ndogo ya wanajeshi.

Russia inatuma wanajeshi ambao hawana mafunzo ya kutosha

Wanajeshi wa Russia wakishiriki karika gwaride na kuonyesha kuunga mkono vita vinayoendelea nchini Ukraine July 11, 2022
Wanajeshi wa Russia wakishiriki karika gwaride na kuonyesha kuunga mkono vita vinayoendelea nchini Ukraine July 11, 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, amesema Alhamisi kwamba “Russia inaendelea kutuma maelfu ya wanajeshi kupigana. Hawajapokea mafunzo ya kutosha lakini makamanda wao hawahitaji wawe wamepokea mafunzo. Wanatarajia kwamba wanajeshi waliosajiliwa watafanikiwa kupigana katika muda wa wiki chache zijazo lakini watakufa na wengine wapya watatumwa.”

Zelenskyy amesema kwamba Ukraine itabuni kamati maalum kuchunguza uhalifu ambao umetekelezwa na Russia dhidi ya Ukraine na kuhakikisha kwamba kuna operesheni maalum kubaini kwamba Russia inalipia gharama ya vita hivyo.

Amesema kwamba “ugaidi lazima ushughulikiwe kwa nguvu zote kwa kila hali. Katika vita, kwa kuwekewa vikwazo na kisheria.

XS
SM
MD
LG