Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:01

Russia imetikisa Ukraine kwa makombora kadhaa mjini Kyiv, mengi yamenaswa


Wanajeshi wa Ukraine wakitumia mwangaza kutambua ndege zisizokuwa na rubani za Russia katika mji wa Kyiv, Ukraine, May 19, 2023
Wanajeshi wa Ukraine wakitumia mwangaza kutambua ndege zisizokuwa na rubani za Russia katika mji wa Kyiv, Ukraine, May 19, 2023

Russia imeushambulia mji mkuu wa Kyiv nchini Ukraine kwa idadi kubwa ya ndege zisizokuwa na rubani kuwahi kutokea tangu kuanza vita hivyo.

Mashambulizi hayo yametokea wakati Ukraine inajitayarisha kuadhimisha kuanzishwa kwa taifa hilo.

Meya wa Kyiv, Vitali Klitscho amesema kwamba mtu mmoja ameuawa kutokana na mashambulizi hayo ya usiku wa kuamkia leo.

Jeshi la anga la Ukraine limesema kwamba limetungua na kuharibu ndege 50 zisizokuwa na rubani za Russia.

Taarifa zaidi hazijatolewa kuelezea iwapo ndege hizo zisizokuwa na rubani, zote zilikuwa zimeulenga mji wa Kyiv au sehemu nyingine za nchi.

Wakati huo huo, taarifa za kila siku za ujasusi za wizara ya ulinzi ya Uingereza zinasema kwamba vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na serikali ya Russia na makundi ya biashara, wanataka wizara ya uchumi kuwaamuru wafanyakazi kufanya kazi siku sita kwa wiki bila kuongezewa malipo ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi kutokana na vita vyake nchini Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG