Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:26

Russia imeshambulia Ukraine kwa makombora 40, mengi yameharibiwa


Ndege ya kivita ya Russia MiG-31K ikiwa imebeba kombora
Ndege ya kivita ya Russia MiG-31K ikiwa imebeba kombora

Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergrey Lavrov yupo Nairobi Kenya ambapo anatarajiwa kufanya mikutano kadhaa na viongozi wa Kenya kabla ya kuelekea Afrika kusini kwa mkutano wa Brics.

Arkadii Kovalev, amesema kwamba makombora 37 aina ya Kh-101 na Kh- 555 yameharibiwa na mfumo wa ulinzi wa Ukraine.

Makombora hayo yamerushwa na ndege ya Russia, kutoka eneo la bahari la Caspian.

Ndege 29 zisizokuwa na rubani, za Iran, pia zimeharibiwa.

Shambulizi hilo lililodumu kwa saa tano, lilianza saa sita usiku na lililenga kambi za jeshi, na mifumo muhimu.

Hayo yanajiri wakati waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergrey Lavrov yupo Nairobi Kenya ambapo anatarajiwa kufanya mikutano kadhaa na viongozi wa Kenya kabla ya kuelekea Afrika kusini kwa mkutano wa Brics.

Ziara ya Lavrov ni ya nne barani Afrika, tangu Russia ilipoivamia Ukraine na kuanzisha vita, Februari mwaka uliopita.

Lavrov amekutana na rais wa Kenya Dr. William Ruto na viongozi wa bunge la Kenya pamoja na maafisa katika wizara ya mambo ya nje.

Ziara yake ni muhimu kwa Kenya na Russia wakati vita vya Ukraine vinapoendelea.

Ataelekea Afrika kusini kwa kiko cha mawaziri wa Brics – nchi tano zinazoinukia, Brazil, Russia, India, China na Afrika kusini.

Ubalozi wa Russia mjini Nairobi umeitaja Kenya kuwa rafiki wa Russia.

Kenya ni moja ya nchi za Afrika ambazo zinapinga uvamizi wa Russia nchini Ukraiane.

Mwakilishi wa Kenya w kudumu katika Umoja wa Mataifa Mrtin Kimani, wakati alikuwa mwakilishi kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, alionya kwamba uvamizi wa Russia unaweza kutonesha makovu ya vidonda vilivyopona.

Kenya imeshikilia msimamo wa Umoja wa Afrika kwamba kuna haja ya kufanyika mazungumzo kati ya Moscow na Kyiv.

Forum

XS
SM
MD
LG