Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 02, 2024 Local time: 01:48

Russia imekubaliana na Jamhuri ya Congo kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta


Moscow imesema kuwa mradi wa pamoja wa ujenzi wa bomba hilo utaifanya Russia kudhibiti asilimia 90 ya taasisi hiyo.

Russia imekubaliana na ujenzi wa bomba la mafuta huko Jamhuri ya Congo, kwa mujibu wa amri ya serikali iliyochapishwa Jumatatu jioni. Bomba hilo litaunganisha bandari ya magharibi ya Pointe-Noire na mji mkuu wa Brazzaville.

Moscow imesema kuwa mradi wa pamoja wa ujenzi wa bomba hilo utaifanya Russia kudhibiti asilimia 90 ya taasisi hiyo. Masuala ya kiufundi na kiuchumi yataelezewa katika mkataba wa makubaliano.

Russia iliahidi kutoa fedha, vifaa na wafanyakazi kwa ajili ya ujenzi wa bomba pamoja na kujaza mafuta bomba hilo, wakati itakapokuwa muhimu. Jamhuri ya Kongo inatarajiwa kukubaliana na kanuni mbalimbali za afueni ya kodi.

Forum

XS
SM
MD
LG