Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:10

Russia imewakamata watu 9 kuhusiana na kulipuliwa kwa daraja huku Ukraine ikiutaja uchunguzi wa Russia ni ‘upuuzi’


Moto na moshi kwenye daraja linalounganisha Russia na Crimea baada ya kushambuliwa Oct. 8, 2022.
Moto na moshi kwenye daraja linalounganisha Russia na Crimea baada ya kushambuliwa Oct. 8, 2022.

Afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Ukraine amelitaja tangazo la Russia kwamba inachunguza shambulizi dhidi ya daraja linalounganisha Crimea na Russia, kuwa upuuzi.

Maafisa wa usalama wa Russia wamewakamata watu 5 raia wa Russia, raia 3 wa Ukraine na mmoja wa Armenia kuhusiana na tukio la shambulizi kwenye daraja hilo.

Rais wa Russia Vladimir Putin amewalaumu wanajeshi wa Ukraine kwa mlipuko huo.

"Shughuli zote za maafisa wa usalama wa siri wa Russia na kuundwa kwa kamati ya uchunguzi, ni upuuzi mtupu,” amesema msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine Andriy Yusov katika mahojiano na shirika la habari la Ukraine – Suspilne.

Yusov ameitaja kamati ya uchunguzi ya Russia na maafisa wa usalama wa siri kuwa “mifumo bandia inayotekeleza kazi yake kwa maslahi ya rais wa Russia Vladimir Putin, na hatutazungumzia taarifa wanazotoa”.

Makombora zaidi yameangushwa Ukraine na kusababisha vifo

Watu wanapiga picha jumba lenye shughuli za biashara lililoharibiwa na makombora ya Russia mjini Lviv, Ukraine
Watu wanapiga picha jumba lenye shughuli za biashara lililoharibiwa na makombora ya Russia mjini Lviv, Ukraine

Watu saba wameuawa hii leo na 8 kujeruhiwa katika shambulizi la kombora la Russia, lililoangushwa sokoni, katika mji wa Avdiivka, leo jumatano.

Gavana wa eneo la Donetsk Pavlo Kyrylenko amesema kwamba “wanajeshi wa Russia wameshambulia soko lililokuwa na watu wengi,” akiongezea kwamba “hakukuwa na sababu yoyote ya kijeshi.”

Gavana huyo ametoa taarifa kwa vyombo vya habari, ambayo ilikuwa pia na picha za miili ya waliofariki.

Russia imedai kwamba msimamo wa NATO ni dhihirisho kwamba unapigania Ukraine

Russia imesema kwamba matamshi ya katibu mkuu wa muungano wa NATO Jens Jens Stoltenberg kwamba “ushindi wa Russia nchini Ukraine itakuwa ni ushindi dhidi ya nchi zote za muungano huo,” ni dhihirisho kwamba muungano huo unapigania Ukraine.

Papa Francis akihutubia waumini mjini Vatican
Papa Francis akihutubia waumini mjini Vatican

Wakati huo huo, kiongozi wa kanisa la katoliki Papa Francis, ameishutumu Russia kwa kurusha makombora katika miji ya Ukraine, akisema kwamba mashambulizi hayo yamesababisha “kimbunga cha vurugu kwa raia.”

Akihutubia maelfu ya watu katika hotuba yake ya kila wiki kwenye bustani ya St. Peters, Papa Francis ametoa wito kwa “wale walio na uwezo wa kumaliza vita hivyo kufanya hivyo.”

Watu 26 wameuawa kufikia sasa katika mashambulizi ya makombora ya yanayorushwa na Russia kuanzia Jumatatu.

Russia ilivamia Ukraine Februari 24.

XS
SM
MD
LG