Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:15

Rufaa ya Ongwen imetupiliwa mbali na ICC, ataendelea kutumikia kifungo


Dominic Ongwen (katikati) aliyekuwa kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la Uganda la Lord's Resistance Army, akiwa katika mahakama ya ICC Hague, Uholanzi, Dec. 6, 2016.
Dominic Ongwen (katikati) aliyekuwa kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la Uganda la Lord's Resistance Army, akiwa katika mahakama ya ICC Hague, Uholanzi, Dec. 6, 2016.

Mahakama ya rufaa ya uhalifu wa kimataifa ICC, imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa kamanda wa kundi la waasi la Lords resistance Army LRA, la nchini Uganda Dominic Ongwen, na kuhalilisha huku aliyopewa ya miaka 25 gerezani.

Ong'wen alihukumiwa baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya binadamu.

Hukumu hiyo ilitolewa karibu miaka miwili iliyopita baada ya Ongwen kupatikana na hatia katika makosa 61 yaliyokuwa yanamkabidhi, yakiwemo mauaji, unajisi, ndoa za lazima na kusajili Watoto kuwa wapiganaji, kati yam waka 2002 na 2005.

Mawakili wake walikuwa wameasilisha hoja 90 katika rufaa hiyo, kwamba kulikuwa na makosa ya kisheria, kimakakati na ya ukweli wakati wa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi dhidi yake.

Jopo la majaji watano wakiongozwa na Jaji Luz del Carmen Ibanez Carranza, amesema kwamba mahakama ya rufaa imekataa rufaa hiyo na kuidhinisha hukumu ya miaka 25 iliyotolewa dhidi ya Dominic Ongwen.

Kundi la waasi la LRA linaongozwa na Joseph Kony, ambaye ni miongoni mwa viongozi wakubwa wa makundi ya waasi wanaosakwa kote duniani.

XS
SM
MD
LG