Jimbo la Kivu Kaskazini la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa katika mtego wa uasi wa M23 toka mwishoni mwa 2021, huku kundi hilo likitwaa maeneo mengi na kuweka utawala sambamba katika maeneo yanayodhibitiwa.
Kinshasa imeishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 linaloongozwa na Watutsi.
Kigali haijawahi kukiri kuwa wanajeshi wake wamekuwa wakipigana ndani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Lakini ripoti iliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imesema Rwanda inadhibiti operesheni za M23 na kuifanya nchi hiyo kuwajibishwa kwa hatua za M23.
Forum