Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:22

Republican na Democrat wanajadiliana kunusuru serikali kuu kufungwa


Jengo la bunge la Marekani
Jengo la bunge la Marekani

Serikali kuu itaanza kusitisha operesheni zisizo za lazima Ijumaa kama bunge na White House hawawezi kukubaliana juu ya mswada wa matumizi ya muda mrefu au mfupi

Viongozi wa Republican na wa Democrat wanajadiliana bungeni kupata muafaka wakati Rais Donald Trump anaonekana kuachana na tishio lake la kulazimisha serikali kuu kufungwa baadae wiki hii. Baada ya kusema wiki iliyopita atafurahi kuona sehemu ya huduma za serikali kuu zinafungwa kufuatia madai yake ya kutengewa fedha za kujenga ukuta, Rais Trump aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne “tutaona nini kinachotokea. Ni mapema mno kusema. Tunahitaji usalama mpakani.

Serikali kuu itaanza kusitisha operesheni zisizo za lazima Ijumaa kama bunge na White House hawawezi kukubaliana juu ya mswada wa matumizi ya muda mrefu au mfupi. Zaidi ya wafanyakazi 800,000 wa serikali kuu watakaa nyumbani bila malipo au kufika kazini, kitu ambacho hakuna mtu yeyote anataka kukishuhudia ikiwa ni siku chache tu kabla ya Christimass.

Trump anataka dola bilioni tano za kufadhili ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico lakini viongozi wa bunge na baraza la wawakilishi wamekataa.

XS
SM
MD
LG