Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 05:04

Rashia yaendelea kurusha makombora kwenye mji wa Ukraine wa Kharkiv

Wazimamoto wakijaribu kudhibiti moto kwenye jengo la chuo kikuu cha Karazin, mjini Kharkiv, jengo linalodaiwa kushambuliwa hivi karibuni na makombora ya Rashia. Picha ya AFP, Machi 2, 2022
Wazimamoto wakijaribu kudhibiti moto kwenye jengo la chuo kikuu cha Karazin, mjini Kharkiv, jengo linalodaiwa kushambuliwa hivi karibuni na makombora ya Rashia. Picha ya AFP, Machi 2, 2022

Maafisa wa Ukraine wanasema Rashia imeendelea kurusha makombora kwenye maeneo ya makazi na majengo ya serikali katika mji wa pili kwa ukubwa wa Kharkiv leo Jumatano.

Video iliyotolewa na wizara ya Ukraine ya hali ya dharura imeonyesha makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani mjini Kharkiv yakichomeka, huku wazima moto wakijaribu kuzima moto huo.

Idara ya dharura ya Kharkiv imesema baadaye kwamba watu watano waliuawa leo Jumatano katika mashambulizi ya makombora katika mnara wa Babi Yar mahali ambako kulitokea mauwaji ya watu elfu 33 yaliyofanywa na wanazi.

Jumanne, watu 6 waliuawa katika shambulio la kombora dhidi ya jengo la kikanda la serikali mjini Kharkiv.

XS
SM
MD
LG