Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:24

Rapper wa Afrika Kusini auwawa Durban


Wanawake wa Afrika Kusini wakiandamana nje ya Krugersdorp, Afrika Kusini, kupinga ghasia na ,mauaji Jumatatu, Agosti 1, 2022.
Wanawake wa Afrika Kusini wakiandamana nje ya Krugersdorp, Afrika Kusini, kupinga ghasia na ,mauaji Jumatatu, Agosti 1, 2022.

Mmoja wa wasanii wa rap nchini Afrika Kusini, Kiernan Forbes, anayejulikana kama AKA, ameuawa kwa kupigwa risasi nje ya mgahawa ulioko kusini mashariki mwa jiji la Durban, familia yake ilisema Jumamosi.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 35 alishinda tuzo nyingi za Afrika Kusini, pia aliteuliwa mara kadhaa kwenye Tuzo ya Black Entertainment Television (BET) nchini Marekani, na aliwahi kuteuliwa kwa Tuzo ya Muziki ya MTV Europe.

"Kwa huzuni kubwa tunatangaza kuondokewa na mwanetu mpendwa," wazazi wake Tony na Lynn Forbes walisema katika taarifa iliyotumwa kwenye akaunti ya Twitter ya AKA. "Mwanetu alipendwa, na alirudisha pia upendo huo"

Alipigwa risasi Ijumaa usiku pamoja na mwanamume mwingine walipokuwa wakitembea kuelekea gari lao kutoka kwenye mkahawa.

Inadaiwa walifatwa na washukiwa wawili waliokuwa na silaha na kuwapiga risasi wakiwa karibu," polisi walisema katika taarifa.

Alipangiwa kutumbuiza katika klabu Ijumaa usiku, kulingana na meya wa jiji la Durban, Mxolisi Kaunda.

XS
SM
MD
LG