Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:50

Ramaphosa asema kuongezeka kwa umaskini Afrika Kusini hakukubaliki


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa amesema hali ya sasa ya nchi hiyo, ya umaskini uliokithiri, ukosefu wa ajira, na kutokuwa na usawa haikubaliki.

Ramaphosa ameeleza hayo wakati wa hotuba yake kuhusu hali ya kitaifa.

Rais Ramaphosa amesema nchi inahitaji mageuzi ya msingi wakati akitoa hotuba yake Alhamisi.

“ Kama kuna kitu ambacho wote tutakubaliana, ni hali ya sasa ya nchi tuliyonayo ya umasikini mkubwa, ukosefu wa ajira na kutokuwa na usawa haikubaliki na haiwezi kuendelea,” ameeleza kiongozi huyo.

Kutokana na ajira zinazohitajika ili kuwatoa mamilioni ya watu kutoka kwenye umasikini , Afrika kusini imejitahidi kubadilisha ukosefu wa usawa wa kiuchumi uliobuniwa chini ya utawala wa wazungu wachache.

Mwezi julai mwaka 2021 ziliibuka hasira juu ya umasikini unaoendelea karibu miongo mitatu baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi.

Kufuatia ripoti za uporaji , uchomaji moto, zaidi ya watu 300 walikufa na kulitokea uharibifu wenye thamani kubwa ya pesa.

Ramaphosa pia amesema msaada wa kijamii ulioanzishwa mwanzoni mwa janga la dunia pia utaongezwa.

XS
SM
MD
LG