Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:59

Rais Xi apongeza 'maendeleo' yaliyopatikana katika mazungumzo na Waziri Blinken


Rais wa China Xi Jinping akiongoza mazungumzo kati ya China na Marekani.
Rais wa China Xi Jinping akiongoza mazungumzo kati ya China na Marekani.

Rais wa China Xi Jinping amepongeza ‘maendeleo’ katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Beijing siku ya Jumatatu, mawasiliano ya mwisho katika ziara adimu iliyolenga  kuhakikisha mivutano kati ya mataifa yenye nguvu haibadiliki na kuwa mizozo.

Blinken ambaye ni kiongozi wa kwanza katika wadhifa wake kukutana na kiongozi wa China tangu mwaka 2018, awali alisogea kuelekea kwa Xi na kuunyoosha mkono wake kwenye jumba maarufu la Great Hall of the people, eneo ambalo wachina mara nyingi wanalitumia kukutana na viongozi wa dunia, hii ikionyesha ishara nzuri ya mwelekeo wa kidiplomasia.

Takriban dakika 30 za mkutano wao zinaweza kufanikisha mkutano baina ya Xi na rais wa Marekani Joe Biden baadae mwaka 2023.

Biden na Xi mara ya mwisho walikutana pembeni ya Mkutano wa G20 huko Bali, Indonesia mwezi Novemba, wakiahidi mawasiliano zaidi , ingawa uhusiano tangu wakati huo umeshuka kuhusu maswala ya Taiwan hadi wasiwasi wa kijasusi.

Rais wa China anaeleza:“ Mkurugenzi Wang Yi na msimamizi wa maswala ya serikali Qin Gang wamekutana au kufanya mazungumzo na wewe kwa kirefu , na kiukweli, pande zote mbili wamekuwa na mazungumzo ya wazi na kina. China imeweka msimamo wetu wazi, na pande zote mbili zimekubali kufuatilia maelewano ya pamoja ambayo rais Biden na mimi tulikuwa tumefikia huko Bali. Pande hizo mbili pia zimepiga hatua na kufikia makubaliano katika maswala kadhaa. Hii ni nzuri sana. Mawasiliano kati ya serikali na serikali yanapaswa kuwa msingi wa kuheshimiana na uaminifu. Natumaini kwamba kupitia ziara hii, waziri utatoa mchango chanya zaidi katika kuleta utulivu kati ya uhusiano wa china na Marekani.

Baada ya kukutana na Xi, Blinken alisisitiza umuhimu wa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja ya ngazi ya juu na pande zote ‘zilikubaliana kuhusu haja ya kuboresha uhusiano.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken anasema:“ Hapa Beijing nimekuwa na mawasiliano muhimu na rais Xi Jinping , nimekuwa na majadiliano ya wazi, muhimu na yenye kujenga na wenzangu Wang Yi na msimamizi wa maswala ya serikali Chen Gong. Ninashukuru mapokezi ya wenyeji wetu . katika kila Mkutano nimesisitiza kuhusu uhusiano wa moja kwa moja na mawasiano thabiti katika kiwango cha juu ni njia nzuri kukabiliana na tofauti zetu na kuhakikisha kwamba ushindani hauwezi kuwa ghasia.

Forum

XS
SM
MD
LG