Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:24

Rais wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela

Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye wakati huo alikuwa rais wa Mauritania, akisubiri kuwasili kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye uwanja wa ndege wa Nouakchott, Mauritania, Julai 2, 2018.
Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye wakati huo alikuwa rais wa Mauritania, akisubiri kuwasili kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye uwanja wa ndege wa Nouakchott, Mauritania, Julai 2, 2018.

Rais wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa mzunguko haramu wa  fedha na utajiri haramu.

Rais wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa mzunguko haramu wa fedha na utajiri haramu.

Abdel Aziz aliiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa muongo mmoja baada ya kuingia madarakani katika mapinduzi ya mwaka 2008 na alikuwa mshirika wa nchi za Magharibi akipambana na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo la Sahel. Alikuwa kwenye kesi tangu mwezi Januari na alikanusha madai ya ufisadi.

Mahakama ilimkuta Abdel Aziz na hatia ya mashtaka mawili kati ya 10 Jumatatu jioni kufuatia uchunguzi wa madai ya ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi.

Mmoja wa mawakili wake aliita uamuzi huo hukumu ya kisiasa inayomlenga mtu na familia yake. Waendesha mashtaka walisema hukumu ya mkuu huyo wa zamani wa nchi ilikuwa ya kihistoria.

Forum

XS
SM
MD
LG