Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 03:13

Rais wa zamani wa Honduras, ahukumiwa miaka 45 kwa ulanguzi wa dawa za kulevya


Rais wa zamani wa Honduras, Juan Orlando Hernandez, Jumatano mjini New York, amehukumiwa kifungo cha miaka 45 katika gereza la Marekani kwa kuwasaidia walanguzi wa dawa za kulevya waliotumia jeshi la Hondura na polisi wa taifa kusafirisha kiasi kikubwa cha kokeini kuingiza Marekani.

Hernandez, 55, alitawala Honduras, akiwa mshirika wa Marekani katika Amerika ya Kati, kutoka 2014 hadi 2022, akitumikia mihula miwili.

Alikamatwa nyumbani kwake katika mji mkuu, Tegucigalpa, miezi mitatu baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 2022 na kupelekwa Marekani mwezi Aprili mwaka huo.

Kaka yake, Juan Antonio “Tony” Hernandez, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani mwaka 2021 kwa mashtaka kama hayo yanayohusiana na dawa za kulevya.

Waendesha mashitaka walidai kuwa Hernandez alishirikiana na walanguzi wa dawa za kulevya toka 2004, akipokea rushwa ya mamilioni ya dola.

Forum

XS
SM
MD
LG