Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:15

Rais wa Tunisia aahidi marekebisho hivi karibuni


Waandamanaji kwenye mji mkuu wa Tunisia wa Tunis
Waandamanaji kwenye mji mkuu wa Tunisia wa Tunis

Rais wa Tunisia Kais Saied Aljhamisi amesema kwamba anafuata ratiba ya moja kwa moja kuelekea marekebisho ya kisiasa ili kumaliza ukosoaji mkubwa wa ndani na nje ya nchi.

Ukosoaji huo ulioanza baada ya kuvunja baraza la mawaziri, kusitisha shughuli za bunge, wakati akijitwika madaraka yote miezi mmne iliyopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Saied hata hivyo hajaeleza muda atakaochukua kufanya hivyo ili kumaliza hali ya dharura iliyopo nchini humo, pamoja na kuurejesha utawala wa kidemokrasia. Saied wakati akifanya kikao na serikali aliyoiteua, amesema kwamba wanafanya kazi usiku na mchana wakizingatia matakwa ya watu wa Tunisia.

Wiki iliyopita maelfu ya watu wa taifa hilo waliandamana karibu na majengo ya bunge wakati wakidai kufunguliwa tena kwa bunge, wakati mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yakiomba hali ya kawaida irejeshwe ili kuokoa uchumi wa taifa hilo,kama ilivyopangwa na IMF.Saied amekuwa akitetea hatua yake kwa kusema kwamba ndiyo njia pekee ya kumaliza migogoro ya kisiasa pamoja kukwama kwa uchumi nchini humo.

XS
SM
MD
LG