Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:05

Rais mpya aapishwa Taiwan


Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, anayeungwa mkono na chama ambacho kina historia ya kuipinga China, ametawazwa hii leo Ijumaa na kuahidi kwamba atatafuta amani kati ya nchi yake na Beijing.

Hata hivyo, Rais huyo amekataa kufanya mazungumzo, jambo ambalo huenda likachangia kuzorota zaidi kwa uhusiano ambao ulikuwa umeimarika kwa miaka nane.

Ing-Wen, ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Taiwan, alisema kwenye hotuba ya hii Ijumaa kwamba atatafuta amani. Rais huyo haungi mkono kujitangaza rasmi kwa Taiwan kuwa huru kutoka China, wala kuungana na nchi hiyo ambayo imekuwa hasimu wa kisiasa wa kisiwa hicho kwa miaka 70.

Hata hivyo, msomi huyo wa sheria mwenye umri wa miaka 59, alipuuza onyo iliyotolewa na Beijing kumtaka akubali kufanya mazungumzo huku Beijing ikishilia kuwa Taiwan na China ni taifa moja.

XS
SM
MD
LG