Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameyashutumu mataifa tajiri kwa kutupa silaha Afrika, ambazo zinaishia mikononi mwa wahalifu na wanamgambo.
Akizungumza kwenye mkutano kuhusu ulinzi amani mjini Abuja Bw.Jonathan alisema uuuzaji wa silaha kwa Afrika na mataifa yaliyoendelea kiviwanda ni moja ya matatizo makubwa ya bara hilo.
Bw.Jonathan pia alitishia kutopeleka majeshi ya Nigeria kwenye mpango wa kulinda amani wa umoja wa mataifa mpaka taasisi hiyo ya dunia itakapobadili sheria za walinda amani.