“Hali” katika mkoa wa Cabo Delgado imeimarika kwa “kampuni hiyo kuanzisha tena shughuli zake muda wowote,” Nyusi aliuambia mkutano kuhusu madini na nishati mjini Maputo.
TotalEnergies ilisitisha mradi wake wa kuchimba gesi wa dola bilioni 20 miaka miwili iliyopita baada ya shambulio baya katika mji wa Palma, mji wa pwani na kitovu cha gesi.
Jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Cabo Delgado, linakabiliwa na uasi unaoendeshwa na wanamgambo wenye uhusiano na kundi la kigaidi la Islamic State.
Uasi huo wa miaka mitano uliua watu 4,683, nusu yao wakiwa raia, na kuwalazimisha watu milioni 1 kuhama makazi yao.
Mkurugenzi mtendaji wa TotalEnergies Patrick Pouyanne alifanya ziara nchini Msumbiji mwezi Februari kujadili masharti ya kuanzisha tena shughuli za kampuni hiyo.