Rais wa mpito wa Chad, Mahamat Idriss Deby, ametishia kuiondoa nchi hiyo ya Afrika ya Kati kutoka kwenye kikosi cha kimataifa cha ulinzi, ambacho alisema kimeshindwa katika jukumu lake la kukabiliana na makundi ya waasi katika eneo la Ziwa Chad.
Deby alitoa kauli hiyo Jumapili wakati wa ziara yake katika eneo hilo, ambalo liko magharibi mwa Chad na pia Nigeria, Niger na Cameroon. Takriban wanajeshi 40 wa Chad waliuawa katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram mwishoni mwa Oktoba.
Akitangaza kuanzishwa kwa operesheni dhidi ya washambuliaji hao, Deby alisema anafikiria kujiondoa kwenye Kikosi Maalum cha Kimataifa cha Kuratibu Kazi (MNJTF), kinachoundwa na wanajeshi kutoka nchi zinazopakana na Ziwa Chad.
Forum