Rais wa Misri Jumatano alikutana na kiongozi wa kijeshi wa Sudan kwa mazungumzo yanayoangazia uhusiano kati ya majirani hao wawili wa Afrika.
Rais Abdel Fattah el-Sissi alimpokea Jenerali Abdel-Fattah Burhan, mkuu wa Baraza la Utawala nchini Sudan katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cairo.
Viongozi hao wawili walikagua gwaride la heshima katika ikulu ya Cairo kabla ya kukaa kujadili masuala ya nchi zao mbili, kulingana na televisheni ya serikali ya Misri.
Mazungumzo hayo huenda yakajumuisha mzozo wa mataifa hayo mawili na Ethiopia kuhusu bwawa kubwa ambalo linajengwa kwenye Mto Blue Nile. Nchi hizo mara kwa mara zimeshindwa kufikia makubaliano ya pande tatu na Ethiopia juu ya kujazwa na uendeshaji wa bwawa la Grand Renaissance la Ethiopia.