Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 05:09

Rais wa Korea Kusini afikishwa mahakamani


Rais wa Korea Kusini, aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumamosi kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi muhimu ambayo itaamua kuhusu kuongeza muda wake wa kuzuiliwa huku wapelelezi wakichunguza maombi yake ya sheria ya kijeshi yaliyo shindikana.

Wafuasi wa Yoon walikusanyika nje ya mahakama na kuzozana na polisi alipowasili kwa gari, wiki kadhaa baada ya kuliingiza taifa katika machafuko kwa kujaribu u utawala wa kiraia.

Mapendekezo ya rais ya tarehe Desemba 3, ya sheria ya kijeshi yalidumu kwa saa sita pekee, huku wabunge wakipiga kura licha ya yeye kuwaamuru wanajeshi kuvamia bunge.

Baadaye Yoon alishtakiwa na bunge na akakataa kukamatwa kwa wiki kadhaa, akiwa amejificha katika makazi yake yenye ulinzi mpaka alipowekwa kizuizini Jumatano baada ya uvamizi wa alfajiri.

Forum

XS
SM
MD
LG