Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, viongozi hao watatu ambao wameongoza siasa za taifa hilo kwa miongo mitatu iliyopita wanatarajia kikao hicho kuwa mwanzo wa kupunguza mivutano ya kisiasa nchini, kulingana na msemaji wa muda wa Gbagbo.
Takriban watu 3,000 waliuwawa 2010 baada ya Gbagbo kukataa kukubali kushindwa na Ouattara, kabla ya waasi waliokuwa wakiunga Ouattara mkono kuvamia mji mkuu wa Abidjan, na kumkabidhi madaraka. Gbagbo baadaye alishitakiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya jinai kutokana na uhalifu wa kivita lakini akondolewa mashitaka mwaka wa 2019, na kisha kurejea nchini mwaka 2021.
Quattara amesema kwamba kikao hicho hakikuwa cha kawaida, na kwamba vikao vingine sawa na hicho vitafuata. Ivory Coast imeshuhudia utulivu kwa kiasi fulani wakati wa utawala wa Ouattara ingawa watu kadhaa waliuwawa wakati wakati wa uchaguzi wa 2020.