Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alisema Jumanne kwamba Russia, imepokea makombora ya masafa marefu kutoka Iran na kuna uwezekano wa kuyatumia Ukraine ndani ya wiki chache.
Ushirikiano kati ya Moscow na Tehran unatishia usalama mpana wa Ulaya, amesema. Marekani, Ujerumani, Uingereza na Ufaransa, Jumanne ziliiwekea Iran vikwazo vipya, ikiwa ni pamoja na hatua dhidi ya shirika lake la ndege la taifa Iran Air.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi Jumatano amesema Tehran haikuwasilisha kombora lolote la masafa ya mbali kwa Russia na vikwazo vilivyowekwa na Marekani na nchi tatu za Ulaya dhidi ya Iran si suluhu.
Forum