Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:31

Rais wa Iran kuapishwa Agosti bungeni


Rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian, ataapishwa bungeni mapema mwezi Agosti kuwa rais wa tisa wa Jamhuri ya Kiislamu, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti Jumapili.

“Sherehe za kuapishwa kwa rais zitafanyika Agosti 4 au 5,” limesema shirika rasmi la habari la IRNA, likimnukuu Mojtaba Yosefi, afisa wa bodi ya wabunge.

“Rais atakuwa na siku 15 za kutaja majina ya mawaziri wake ataowapendekeza bungeni kwa ili kupigiwa kura ya Imani nao.”

Marais wateule wa Iran wanatakiwa kula kiapo mbele ya bunge kabla ya kuchukua madaraka rasmi.

Hafla ya kuapishwa inafanyika baada ya rais mteule kupata ridhaa rasmi na kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu.

Rais wa Iran sio mkuu wa nchi, na mamlaka ya mwisho ni ya kiongozi mkuu wadhifa unaoshikiliwa na Ayatollah Ali Khamenei kwa kipindi cha miaka 35 iliyopita.

Forum

XS
SM
MD
LG