Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:20

Rais wa DRC kuzuru China, mikataba ya biashara ya madini yatarajiwa kusainiwa


FILE PHOTO: Rais Felix Tshisekedi
FILE PHOTO: Rais Felix Tshisekedi

Rais wa nchi yenye utajiri wa madini ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC Felix Chisekedi atakwenda  china kuanzia Mei 24 hadi 29 na anatarajiwa kukutana na rais She Jimping kutathmini na kutia saini makubaliano muhimu ya kibiashara.

Mkutano huo utafungua njia kwa nchi hizo mbili kufikia makubaliano ya mpango wa dola bilioni 6 kwa ajili ya miundombinu kwa madini na wawekezaji wa china. Ziara hiyo ilitangazwa na wizara ya mambo ye nje ya china jumatatu.

Chisekedi ameiagiza serikali yake katika mkutano wa baraza la mawaziri Mei 19 kuendelea na mazungumzo ya mpango huo na mshirika wake China baada ya serikali ya DRC na wadau wengine kuonyesha msimamo wao , taarifa ya serikali ya DRC imesema.

Amewaambia mawaziri kwamba kikosi kazi kitafuatilia makubaliano ambayo yamewasilishwa hadi kufikai mwisho , na kuwezesha majadiliano na washirika wa China kuanza katika siku za usoni.

Wakati wa ziara yake ya China , wakuu hao wawili wa nchi watafanya mazungumzo na kuhudhuria sherehe za utiaji saini nyaraka za ushirikiano , wizara ya mambo ya nje ya china imesema.

XS
SM
MD
LG