Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 21:34

Rais wa Comoro hayupo tena hatarini baada ya shambulizi la Ijumaa


Rais wa Comoros Azali Assoumani kwenye piccha ya maktaba.
Rais wa Comoros Azali Assoumani kwenye piccha ya maktaba.

Rais wa Comoro Azari Assoumani hayupo tena hatarini baada ya kujeruhiwa katika tukio la kuchomwa kisu Ijumaa, na afisa wa polisi mwenye umri wa miaka 24 ambaye alipatikana akiwa amekufa kwenye rumande, maafisa wa usalama wamesema Jumamosi.

Shambulizi hilo lilifanyika Ijumaa saa nane za mchana kwenye mji wa Salimani Itsandra, uliopo kaskazini mwa mji mkuu, Moroni. Azari alikuwa anahudhuria mazishi wakati wa tukio hilo, ambalo lengo lake halijadhibitishwa. Ripoti zimeongeza kusema kuwa mshambuliaji kwa jina Ahmed Abdou, alichukua likizo kazini Jumatano, kabla ya kutekeleza shambulizi hilo Ijumaa.

Baada ya shambulizi hilo, alikamatwa na kuwekwa kizuizini, lakini akapatikana akiwa amekufa Jumamosi asubuhi, pale wachunguzi walipoenda kumuangalia. Taarifa hizo zimetolewa na mwendesha mashitaka wa umma akiongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini nia ya shambulizi hilo ,na pia kilichosababisha kifo cha mshambuliaji huyo.

Assoumani aliapishwa Mei mwaka huu kama rais kwa muhula wa nne, kufuatia uchaguzi mkali wa Januari, ambao upinzani ulidai ilijawa na dosari, suala ambalo maafisa wa uchaguzi walikanusha.

Forum

XS
SM
MD
LG