Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 06, 2025 Local time: 16:26

Rais wa Colombia asitisha mashauriano na wanamgambo


Rais wa Colombia, Gustavo Petro, Ijumaa amesema kwamba anasitisha mashauriano ya amani na wanamgambo  wa National Liberation Army (ELN) siku moja baada ya ghasia kati ya makundi yenye silaha kaskazini mashariki na kusababisha vifo vya takriban watu 30.

Vurugu hizo zilitokea katika eneo la Catatumbo, kwenye mpaka na Venezuela, ambako makundi hasimu yamekuwa yakipigana kwa miaka mingi kudhibiti biashara ya dawa za kulevya aina ya kokeni.

Mapigano ya karibuni yaliwahusisha waasi wa mrengo wa kushoto wa ELN, kundi kubwa zaidi kati ya makundi yenye silaha ambalo linafanya harakati zake nchini Colombia, dhidi ya wapinzani wa Marxist Revolutionary Armed Forces of Colombia (FARC), ambacho kilitia saini mkataba wa amani na nchi hiyo mwaka 2016 baada ya zaidi ya miaka 50 ya vita.

Rais Petro aliishutumu ELN kutenda uhalifu wa kivita, na kueleza kuwa sababu ya kusimamisha mazungumzo na kundi hilo, ni kwa vile ELN haionyeshi nia ya kuleta amani.

Forum

XS
SM
MD
LG