Matamshi yake yanalenga vikwazo vya nchi za magharibi dhidi ya Russia kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.
Akizungumza katika kongamano mjini Hainan, Xi, amesema kwamba China inaheshimu sana uhuru na mipaka ya nchi zote na haiwezi kuingilia mambo ya ya ndani ya nchi hizo.
Amesema kwamba kuna haja ya kujenga mfumo thabithi wa usalama na wa kudumu, na wala sio kujenga mfumo wa usalama wa taifa kwa kuzingatia ukosefu wa usalama katika nchi zingine.
China imeendelea kuwa na uhusiano mzuri na Russia, na haijashutumu uvamizi wa Russia nchini Ukraine, huku ikishutumu vikwazo vikali ambavyo nchi za magharibi zimeiwekea Russia.