Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 03:06

Rais wa Afrika Kusini yuko katika mazungumzo ya kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa


Chama cha ANC kimeonyesha kuegemea upande wa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itavileta pamoja vyama vingi vya siasa katika makubaliano mapana, badala ya muungano wa moja kwa moja na upinzani mkuu, Democratic Alliance, au DA.
Chama cha ANC kimeonyesha kuegemea upande wa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itavileta pamoja vyama vingi vya siasa katika makubaliano mapana, badala ya muungano wa moja kwa moja na upinzani mkuu, Democratic Alliance, au DA.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alikuwa akikutana na maafisa wakuu wa chama cha African National Congress ili kuamua jinsi ya kuunda serikali baada ya chama hicho kupoteza utawala wake wa miaka 30

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alikuwa akikutana na maafisa wakuu wa chama cha African National Congress siku ya Alhamisi ili kuamua jinsi ya kuunda serikali baada ya chama hicho kupoteza utawala wake wa miaka 30 na kuwa katika mkwamo baada ya uchaguzi.

Kamati ya Kitaifa ya Utendaji ya chama hicho ilikuwa ikikutana mjini Johannesburg ili kushughulikia mgawanyiko kati ya safu za chama kuhusu mwelekeo upi wa kuchukua.

ANC kilipoteza wingi wake wa muda mrefu katika kura ya wiki iliyopita lakini kimesalia kuwa chama kikubwa zaidi, sasa kinahitaji aina fulani ya makubaliano na wengine ili kuiendesha nchi iliyoendelea zaidi kiviwanda barani Afrika.

ANC imeonyesha kuegemea upande wa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itavileta pamoja vyama vingi vya siasa katika makubaliano mapana, badala ya muungano wa moja kwa moja na upinzani mkuu, Democratic Alliance, au DA.

Tunataka kumleta kila mtu aingie ndani. Katibu Mkuu wa ANC Fikile Mbalula alisema kabla ya mkutano wa Alhamisi, ambao unaweza kudumu siku nzima. Mbalula alisema serikali ya umoja wa kitaifa inapendekezwa kwa NEC ili iamue, lakini alitarajia kutakuwa na mijadala na kutoelewana.

Forum

XS
SM
MD
LG