Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:41

Rais Trump ametoa msamaha kwa wanajeshi waliokutwa na hatia kazini


Rais wa Marekani, Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald Trump

Rais Trump alirudisha cheo cha Navy Seal ambaye alishushwa wadhifa baada ya kupiga picha na maiti huko Iraq. Rais alitoa pia msamaha kwa mwanajeshi mwenye nyota moja Clint Lorance pamoja na ofisa wa jeshi Meja Mathew Golsteyn

Rais wa Marekani Donald Trump anaripotiwa kupinga ushauri wa maafisa wa ulinzi, ambapo Ijumaa alitoa msamaha kwa maafisa wawili wa jeshi walioshutumiwa kwa uhalifu wa vita nchini Afghanistan, akiwemo mmoja ambaye alikutwa na hatia na mwingine ambaye anasubiri hukumu.

Rais Trump pia alirudisha cheo cha Navy Seal ambaye alishushwa wadhifa baada ya kupiga picha na maiti huko Iraq. Rais alitoa pia msamaha kwa mwanajeshi mwenye nyota moja Clint Lorance na kwa ofisa wa jeshi Meja Mathew Golsteyn.

Lorance aliamrisha wanajeshi wake kuwafyatulia risasi wanaume watatu wasiokuwa na silaha na alikutwa na hatia ya mauaji bila kukusidia. Golsteyn alikuwa anasubiri hukumu kwa shutuma za mauaji ya mtu aliyeshukiwa kutengeneza bomu Afghanistan mwaka 2010. Kesi yake ilikuwa ianze mwakani.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Trump pia amerejesha wadhifa wa mkuu wa kitengo maalumu kinachoongoza mapigano, Edward Gallagher, ambaye alishushwa cheo baada ya kupiga picha na maiti ya mwanamgambo adui, lakini alikutwa hana hatia ya mauaji ya kukusudia na jaribio la mauaji.

Kwa mujibu wa repoti ya kituo cha televisheni cha CNN, maafisa wa ulinzi walimuonya Rais Trump kwamba msamaha huo utaumiza uadilifu wa mfumo wa sheria jeshini. Hata hivyo White House iliutetea uamuzi wake.

XS
SM
MD
LG