Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 07:02

Rais Trump amemfukuza kazi kaimu Mwanasheria Mkuu Marekani


Aliyekuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Sally Yates.
Aliyekuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Sally Yates.

Rais wa Marekani Donald trump amemfukuza kazi jumatatu usiku kaimu Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Sally Yates, kutoka utawala wa Obama ambaye jumatatu aliagiza idara ya mahakama kutounga mkono amri ya Rais Donald Trump ya kuzuia kwa muda marufuku ya safari kutoka nchi saba nyingi za ki-islam.

Taarifa ya Ikulu ya Marekani-White House ilisema Yates aliisaliti wizara ya mahakama kwa kukataa kutekeleza amri ya sheria iliyobuniwa ili kuwalinda raia wa Marekani. Taarifa pia ilisema Yates ni mdhaifu kwenye masuala ya mipaka na pia mdhaifu kwa wahamiaji haramu.

Nafasi yake itachukuliwa kwa muda na Dana Boente, mwanasheria kutoka jimbo la Virginia, ambaye atahudumu mpaka baraza la seneti litakapoidhinisha uteuzi wa seneta wa jimbo la Alabama, Jeff Sessions aliyeteuliwa na Rais Trump kuwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani.

XS
SM
MD
LG